Kamati ya Fedha na Uongozi ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imefanya ziara ya kutembelea maeneo yaliyopendekezwa kujengwa ofisi itakayotumika na Wahandisi wa Halmashauri na Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kipindi cha utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa Miji Tanzania (TACTICS)
Akizungumza katika majumuisho ya ziara hiyo yalifanyika Leo Machi 25, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, Naibu Meya wa Manispaa, Mhe. Sixmund Lungu amesema kuwa baada ya kuona uhalisia wa maeneo hayo kamati imeridhia ofisi hiyo kujengwa eneo la ofisi za Idara ya Ujenzi lililopo Skoya, Kata ya Vigaeni.
Amesema kuwa ziara hiyo imesaidia kuleta uelewa kwa kamati, hivyo amewataka wataalum kuona namna bora ya kuliendea jambo hilo katika hatua zinazofuata ili mradi uweze kuanza kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi.
Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na kiwanja Na.132/1 kitalu 1 kilichopo kata ya Vigaeni na eneo la Ofisi za Ujenzi lililopo Skoya Kata ya Vigaeni.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.