Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile, leo Januari 21,2025, ameiongoza Kamati ya Fedha na Uongozi kutembelea miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya 185m/= (185,127,000/= ) kwa lengo la kuona namna inavyoendelea.
Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Ndile ameisisitiza timu ya menejimenti (CMT) kuhakikisha usimamizi mzuri wa mapato ya soko kuu Mtwara ili yaweze kutumika kuimarisha miundombinu na shughuli zingine za maendeleo.
Aidha, amewataka Maafisa afya na Kushirikiana na wafanyabiashara soko kuu la Mtwara (WABISOKO) kuimarisha hali ya usafi sokoni hapo ili kujiepusha na mlipuko wa magonjwa.
Pia ametoa maagizo kwamba jengo la ofisi ya Ardhi lililopo Kata ya Rahaleo kuanza kutumika ifikapo Februari mosi, 2025 ili kurahisisha huduma na kufanya nyaraka za Serikali zitunze sehemu salama.
Vilevile Mstahiki Meya amewapongeza wasimamizi wa miradi baada ya kuridhishwa na usimamizi wao mzuri.
Miradi hiyo inayotekelezwa kupitia Fedha za mkusanyo ya mapato ya ndani iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa matundu mawili ya vyoo vya walimu, matundu nane ya vyoo vya wanafunzi na ukarabati wa choo shulebya Msingi Chuno, Utengenezaji wa Viti na Meza Sekondari ya Chuno,
Miradi mingine ni Utengenezaji wa Viti, Meza na ukarabati wa Shulebya Sekondari ya Mangamba,Ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje Zahanati Mtawanya,Utengenezaji wa Viti na Meza Shule ya Sekondari Umoja,Ukarabati na uingizaji wa Umeme Soko Kuu na Ukamilishaji wa Ujenzi wa Ofisi ya Ardhi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.