Wajumbe wa Kamati ya fedha na Uongozi Manispaa ya Mtwara-Mikindani leo April 21,2022 wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo yenye gharama ya shilingi Milioni Mia tisa (900,000,000) inayoendelea kutekelezwa ndani ya Manispaa hii.
Miradi iliyotembelewa ni Pamoja na mradi wa ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje , Maabara na kichomea taka Zahanati ya Ufukoni (9250,000,000), ujenzi wa eingo la kujifungulia Zahanati ya Mbawala chini (60,000,000) Pamoja na ujenzi wa nyumba ya mtumishi zahanati ya Mtawanya (30,000,000).
Miradi mingine ni Pamoja na ujenzi wa shule ya Sekondari ya mfano Likombe (470,000,000), ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari Umoja (40,000,000), ujenzi wa ofisi ya Mipango Miji (50,000,0000 pamoja na ukarabati wa machinjio Chuno.
Wajumbe hao wameridhika na Maendeleo ya Miradi hiyo na wamewasisitiza wataalamu kusimamia miradi hiyo kwa ukaribu ili iweze kukamilika kwa wakati na kwenye ubora unaotakiwa
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.