Kamati ya huduma za Jamii Manispaa ya Mtwara-Mikindani ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mussa Namtema (Diwani wa Kata ya Chikongola) Leo Oktoba 25,2024 imefanya ziara ya kuona na kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwa ni ziara ya kawaida ya kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025
Katika ziara hiyo Kamati hiyo imeridhishwa na uendeshaji na utunzaji wa mazingira unaofanywa na Kampuni ya makaa ya mawe Bandarini (Ruvuma Coal).
Aidha imeahidi kushughulikia changamoto za watoto wenye mahitaji maalumu wanaosoma Shule ya Msingi ya Rahaleo pamoja na kumsisitiza Mkurugenzi kutengeneza vitanda ili wanafunzi hao waanze kuishi kwenye bweli lililojengwa kwa ajili yao shuleni hapo.
Kamati hiyo pia imemuonya mfanyabiashara wa chakula eneo la Magomeni (Mpemba One ) kuacha kutiririsha maji machafu kwenye mfereji wa maji ya mvua kwa kuwa ni uchafuzi wa mazingira na inaleta kero kwa wananchi wanaoishi jirani na maeneo hayo.
Aidha imemuagiza Afisa Mazingira kuhakikisha anasafisha vizimba ambavyo havitumiki na kuvifunga ili wananchi wasiendelee kutupa taka katika maeneo hayo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.