KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA MACHINJIO CHUNO
Kamati ya Huduma za Jamii, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani leo (23/04/2025) imefanya ziara kwenye Machinjio ya kisasa ya Chuno na kukugua ujenzi wa Zizi lilolojengwa ili kurahisisha uhifadhi wa mifugo kwenye machinjio hiyo.
Kamati hiyo, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Musa Namtema (Diwani kata ya Chikongola) imeshauri Zizi hilo litanuliwe ili kuongeza uwezo wa kupokea mifugo mingi zaidi, ambapo kwa sasa uwezo wake ni kupokea wastani wa ng'ombe 20 wakati Machinjio inahudumia Ng'ombe 20 kwa siku za kawaida hadi Ng'ombe 40 kwa siku za sikukuu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.