Kamati ya huduma za Jamii Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeiagiza Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Jangwani kuitisha Mkutano wa wazazi wa Mtaa wa Dimbuzi kwa ajili ya kuwahamasisha kuchangia upatikanaji wa uji Kwa wanafunzi wanaosoma darasa la awali katika Kituo Shikizi Cha Dimbuzi (Shule mama ya Rwelu)
Agizo hilo limetolewa baada ya kamati hiyo kutembelea darasa la awali la kituo hiko kilichopo Kata ya Jangwani na kubaini kuwa wanafunzi wanaosoma hapo hawapati chakula jambo ambalo linaweza kupelekea watoto kutoshiriki masomo vizuri darasani.
Kamati imetoa maagizo hayo Leo Januari 20,2025 ilipofanya ziara ya robo ya pili ya mwaka 2014/2025 ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa Kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Aidha Kamati hiyo imewasisitiza Wataalamu Kuhakikisha wanawasimamia mafundi waliopata kazi ya ujenzi ili miundombinu ukamilike kwa wakati.
Na Kwa miradi ambayo haijaanza kamati imeiagiza kukamilika Mchakato wa manunuzi ili miradi ianze kutekelezwa.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa matundu ya vyoo matatu Kituo Shikizi Cha Dimbuzi (5,000,000), ujenzi wa zizi la kuhifadhia ng'ombe (3,000,000) katika machinjio ya Chuno pamoja na ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari ya Likombe (40,000,000
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.