Kamati ya Kuthibiti Ukimwi Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani, imesisitiza ushirikiano na Wadau wa Kupambana na Maambukizi ya VVU na UKIMWI ili kufanikisha jitihada za serikali katika kufikia malengo ya dunia ya 95-95-95 katika kupambana na maambukizi ya UKIMWI.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambae pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Sixmund Lungu, ametoa rai hi hiyo wakati wa ziara iliyofanyika leo tarehe 12 Mei, 2025 kwa lengo la kutambuana na wadau na kukumbushana majukumu ya mbalimbali.
Alisema anafahamu fika kwamba wadau wengi wameshindwa kufikia malengo kutokana na kusimama kwa baadhi ya huduma za ukimwi kutokana na tamko la serikali ya Marekani hivyo kwa kushirikiana pamoja malengo yatafikiwa.
Wadau waliotembelewa na kamati hiyo ni Pamoja na USAID kupitia mradi wa 'Kizazi hodari - Southern Zone Activity' Pamoja na Shirika la COCODA.
Mpango wa 95-95-95 ni mkakati wa kimataifa katika mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI (HIV) ulioanzishwa na Umoja wa Mataifa.
Yaani 95% ya watu wote walio na virusi vya HIV wajue hali zao, 95% ya watu walio na virusi wapate matibabu sahihi Pamoja na 95% ya watu walio kwenye matibabu wawe na uwezo wa kuzuia kuenea kwa virusi ‘viral suppression’.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.