Kamati ya Mipangomiji imefanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo soko la Kiyangu (SOKOSELA) ambapo imeiagiza Menejimenti ya Manispaa kuhakikisha inasafisha eneo la ndani la soko hilo (kuvunja vibanda vilivyopo) ili litengenezwe vizuri kwa ajili ya kuwakaribisha wadau waweze kuwekeza kwa shughuli za kiuchumi katika eneo hilo Leo April 22,2025
Diwani wa Kata ya Shangani (Kata ambayo soko hilo lipo) Mhe. Abuu Mohamedi Abdallah amesema kuwa Ofisi ya Kata imeshakutana na wafanybiashara wa soko hilo na kukubaliana kufanyika kwa maendeleo hayo ili soko hilo liweze kutumika vizuri.
Aidha katika ziara hiyo wajumbe pia walitembelea Mangamba (Uwanja wa ndege) kuona eneo lenye mgogoro wa ardhi, eneo la Pentekoste kuangalia eneo linalotarajiwa kuwekwa ofisi ya kuoshea magari, eneo la maghalani pamoja na Ofisi mpya ya Mipangomiji
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.