Kamati ya Mipangomiji Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani leo tarehe 28 Oktoba, 2024, imefanya ziara ya kutembelea eneo linaliendelezwa na mwekezaji AFLII Tanzania (Maarufu kama kwa Mzungu Mji Mwema) ili kukagua Maendeleo ya mradi huo.
Mradi huo wenye ukubwa wa takribani ekari 50 unajumuisha Ujenzi wa shule ya Awali na Msingi, Chuo cha mafunzo kwa wakulima, Nyumba ya kulala wageni (Lodge), Eneo la mapumziko (Recreation Centre), Kituo Cha elimu pamoja na makazi ya watu.
Sambamba na hilo kamati pia imetembelea na kukagua Viwanja vinavyopendelezwa kufutwa - katika mtaa wa Mbae-Mashariki, pamoja na Maeneo ya wazi yanayoombwa kukodishwa mtaa wa Shangani West.
Aidha kamati imetembelea na kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Mipangomiji katika mtaa wa Rahaleo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.