Kamati ya ushauri wafanyakazi wanawake Mkoa wa Mtwara chini ya mwamvuli wa Chama cha Wafanyakazi Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) wamekabidhi vifaa vya usafi katika kituo cha Afya Ufukoni, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni Pamoja na Vitunza taka (Dustbins), squeezers, Brash za choo (Toilet brush) cobweb remover broom, Ndoo maalum za kudekia na Mifagio.
Vifaa vingine ni Viziloea taka (Dustbins), Majemb, mapanga, fyekeo (slashers), na sabuni za maji.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bi. Mwanhamisi Chimbede amesema kuwa lengo la kukabidhi vifaa hivyo ni kuwawezesha watumishi wa kituo hicho kufanya kazi katika mazingira ya usafi.
Kwa upande wa kaimu Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dkt. Zamda Kaisi, ameishukuru kamati hiyo kwa kukabidhi vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kuimarisha usafi katika kituo hicho.
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Mwaka huu yanaendana na kauli mbiu inayosema, wanawake na wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na uwezeshaji.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.