Katika kuunga Mkono juhudi za Serikali na Wananchi katika kutatua changamoto Septemba 18, 2021 Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi Taifa Ndg, Shaka Hamdu Shaka amechangia mifuko 20 ya Saruji katika ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya msingi Kambarage iliyopo katika Kata ya Shangani.
Sambamba na hilo Ndg. Shaka amehaidi kuchangia madawati 20 ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa madawati katika shule hiyo.
“Hizi chanagamoto ni zetu sote, nami sitabaki nyuma nitaleta mifuko 20 ya Saruji kabla sijaondoka lakini pia nitaleta na madawati 20”Amesema Ndg. Shaka
Aidha amewapongeza wananchi wa Kata ya Shanagani kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zilizopo katika Jamii.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.