Wanakikundi wa kikundi cha Maendeleo wakitengeneza sabuni ya maji
Katika kuhakikisha kuwa kaya masikini zinawezeshwa ili ziweze kujitegemea na kujiongezea kipato Manispaa ya Mtwara-Mikindani Kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imeendesha mafunzo ya siku 7 ya ujasiriamali kwa kikundi cha Maendeleo kinachonufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini katika mtaa wa rwelu.
Akiongea kwenye mafunzo hayo desemba 19,2018 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa bi Juliana manyama amesema kuwa, kwa kuwa Serikali inatoa ruzuku ya kila mwezi kwa kaya masikini Idara imeamua kutoa mafunzo kwa walengwa hao ili waweze kujiendesha hata mpango utakapokamilika.
Amesema kuwa pamoja na kutoa mafunzo hayo Manispaa itaendelea kuwapatia ushauri wa kitaalamu na kuwasaidia kupata masoko yaliyopo ndani na nje ya Manispaa ili waweze kuuza bidhaa zao.
Akiongea kwa niaba ya wanakikundi wenzake bi. Mwajuma Lipamba ameishukuru Serikali na Manispaa kwa kuwapatia mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kutengeneza bidhaa bora na kutafuta masoko ili waweze kutoka kwenye umasikini walionao na kujitegemea kama watu wengine.
Mafunzo waliyopatiwa ni pamoja na utengenezaji wa batiki, sabuni ya maji pamoja na sabuni ya kipande na takribani wanavikundi 47 kutoka Kata ya Jangwani, Ufukoni, vigaeni na Rahaleo. wamenufaika na mafunzo hayo na wanaendelea kuwafundisha wenzao. Aidha utoaji wa mafunzo kwa vikundi vingine vya kaya masikini katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali utaendelea katika Kata zingine.
Matukio katika picha
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.