KIKUNDI CHA UFUGAJI WA SAMAKI MTAWANYA CHAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA KUSHIRIKIANA
Kikundi cha ufugaji wa samaki cha Umoja ni nguvu kilichopo Kata ya Mtawanya ambacho kimepata mkopo wa asilimia kumi kutoka Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Shilingi milioni hamsini na sita (56,000,000) kimetakiwa kufanya kazi kwa kushikamana na kushirikiana kwenye kila hatua ya ufugaji ili waweze kupata mazao mengi ya samaki ambayo watayauza na kupata fedha zitakazo wasaidia kurejesha mkopo kwa wakati.
Rai hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile alipoambatana na wajumbe wa kamati ya fedha na Uongozi kwenye ziara ya Ukaguzi wa miradi ya maendeleo robo ya tatu mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Aidha amewataka wanakikundi hao kuwashirikisha wataalamu wa uvuvi kwenye kila hatua ili wapate mafanikio huku akiwasisitiza wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kuendelea kuwasimamia kwa ukaribu ili waweze kurejesha fedha walizokopeshwa.
Mwenyekiti wa kikundi hiko Bi. Hidaya Ally Kichombaki ameihakikishia kamati hiyo kuwa watafanya kazi kwa bidii na kwa kujituma ili waweze kupata samaki wengi watakaowauza na kufanya marejesho .
Kamati iyo pia ilitembelea ujenzi wa hospitali ya halmashauri Mjimwema ambapo walihimiza ushirikishwaji wa wananchi katika mradi huo, ujenzi wa bwalo la chakula shule ya Sekondari ya Naliendele, ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa Mtonya B pamoja na Ujenzi wa matundu ya Vyoo kumi Shule ya Sekondari ya Sino.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.