Baraza la Madiwani la Manispaa ya Mtwara-Mikindani lililoketi Oktoba 25,2018 katika ukumbi wa Manispaa imesikia kilio cha wafanyabiashara na kuridhia kupunguza baadhi ya viwango vya tozo vilivyopo kwenye sheria ndogo mpya ya Manispaa hiyo iliyotangazwa katika gazeti la Serikal la tarehe 27 April,2018
Punguzo hilo limefanyika baada ya wadau na wafanyabiashara kuilalamikia sheria hiyo kuwa viwango vilivyowekwa ni vikubwa ukilinganishia na uhalisia uliopo.
Kutokana na uwepo wa malalamiko hayo ilipelekea wafanyabiashara waliopo eneo la soko kuu Mtwara na stendi kuu ya mabasi kugoma kufungua biashara zao na kusitisha huduma kwa siku mbili mfululizo kuanzia tarehe 24 hadi 25oktoba 2018 wakidai tozo za vibanda iliyopo kwenye sheria ndogo ipunguzwe.
Akizungumza wakati wa kufunga kikao cha baraza la Madiwani Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mwara-Mikindani mhe. Geofrey Mwanichisye amesema kuwa kilio cha wafanyabiashara hao kimesikika na hivyo kikao kimeridhia kimepunguza baadhi ya tozo zilizolalamikiwa kuwa kubwa hususani tozo ya vibanda vya biashara vilivyopo kwenye masoko na stendi kuu ya mabasi.
Amesema kuwa viwango vilivyopitishwa kwenye kikao hicho ni vya mpito na vinaanza kutumika kuanzia Julai mwaka huu hadi Juni 2018 wakati halmashauri ikifanya mapitio upya ya sheria ndogo iliyopitishwa (inayolalamikiwa)
Tozo zilizofanyiwa marekebisho ni pamoja na ushuru wa mabanda makubwa kutoka shilingi 75,000 kwa mwezi hadi shilingi 40,000 kwa mwezi na mabanda madogo kutoka shilingi 50,000 hadi 25,000 kwa mwezi.
Tozo nyingine zilizofanyiwa marekebisho ni pamoja na ushuru wa vizimba vya (matunda na mbogamboga, kuku, bucha, kizimba cha kuzunguka soko ,tumbaku, kizimba cha chai na chakula, kizimba cha samaki pamoja na meza kutoka shilingi 20,000 kwa mwezi hadi 10,000 kwa mwezi), kizimba cha nafaka na gunia kutoa shilingi 50,000 hadi 30,000 kwa mwezi pamoja na stoo iltalipiwa shilingi 30,000 kwa mwezi.
Aidha mwanichisye amewataka wafanyabiashara na wananchi wote wa Mtwara-Miindani kutekeleza wajibu wao kwa kulipa kodi mbalimbali za halmashauri ili kuleta maendeleo na kuwataka viongozi kuzingatia taratibu kanuni na miongozo kwenye maamuzi bila kuangalia itikadi za vyama vyao .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.