Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi ameipongeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kutumia fedha za mapato ya ndani Shilingi milioni thelathini na tatu laki nne (33,400,000) zilizotumika kujenga Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Msikitini uliopo Kata ya Majengo na ameridhia kuizindua Ofisi hiyo kwa kuwa inaenda kuimarisha Utawala bora.
“Niwapongeze kwa kazi kubwa mnayoifanya Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi na timu yako kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuwaletea wananchi Maendeleo nina imani Mungu atawajalia na Mkurugenzi Mhe. Rais ataendelea kukuona”
“ Tumefanya ukaguzi wa jengo hili na tumejiridhisha kuwa jengo limezingatia viwango, sifa na mahitaji ya wananchi “ amesema Ndugu. Ussi
Awali akisoma taarifa ya mradi huo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Majengo Athumani Magambo amesema kuwa uwepo wa Ofisi hiyo itaboresha ustawi wa wananchi kwa kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowagusa wakazi wapatao 1094 wa mtaa huo.
Aidha Magambao ametoa shukrani zake za dhati kwa Uongozi wa Manispaa hiyo kwa kuridhia kutoa fedha za ujenzi wa Ofisi
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.