Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Ismail Ali Ussi amewamwagia sifa Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Mtwara kwa uanzishaji na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na kwa kuzifuata vyema Itifaki za Mwenge hali iliyopelekea miradi yote kukubaliwa.
Ussi ameyasema hayo leo tarehe 26 Mei, 2025, wakati akiaga Mkoa wa Mtwara na kuingia Mkoani Lindi ambapo Mwenge utakimbizwa katika Halmashauri 6 za Mkoa huo.
Aidha, alitumia jukwaa hilo kutoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kwa Amani na Utulivu kama kaulimbiu ya Mwenge mwaka huu inavyojieleza.
Vilevile, aliwataka wananchi kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI, Malaria, Dawa za kulevya na Mapambano dhidi ya rushwa.
Ikumbukwe kwamba Kiongozi hiyo alikabidhiwa Mwenge wa Uhuru tarehe 03 Aprili, 2025 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, Mkoani Pwani na hadi sasa umeshapita mikoa Saba (7) kati ya 31 ya Tanzania bara na Visiwan
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.