Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu. Ismail Ali Ussi amekipongeza kikundi cha vijana cha Wajenzi Enterpreneurs kinachojishughulisha na ujenzi kwa kutumia vizuri fedha za mkopo wa asilimia kumi zilizokopeshwa na Manispaa kupitia mapato yake ndani shilingi milioni thelathini na mbili laki saba (32,700,000) na kuwataka vijana kuhakikisha fedha hizo zinawanufaisha kiuchumi.
Adha amewashukuru Vipngozi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kuwahamasisha vijana kutumia mfumo wa Nest kwenye manunuzi yao lakini pia itawafanya vijana kupata kazi mbalimbali za za ujenzi kupotia mfumo huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ndugu. Ismail Ali Ussi aameyasema hayo leo Mei 25,2025 alipotembelea kikundi hiko kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru
Mwenyekiti wa kikundi hiko ndug. Rasuli Nahembe amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo ulianza mwaka 2023 ukiwa na wanachama sita waliolenga kujikwamua kiuchumi kwa kujiajiri.
Amesema kuwa wakati wanaanzisha mradi huo walikuwa na mtaji wa shikingi milioni saba ((7,000,00) na kwamba hadi kufikia sasa kikundi kina mtaji wa Shilingi milioni thelathini na tisa laki saba (39,700,000) baada ya kupokea mkopo wa asilimia kumi kutoka Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Ndugu. Nahembe amemshukuru Rais wa Jahuri ya Muu
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.