Katika kuhakikisha kuwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani inaendelea kukinga na kutibu maambukizi ya ugonjwa wa Malaria, Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe.Hassan Mtenga amekabidhi vyandarua 200 kwa Mganga Mkuu wa Manispaa Dkt. Elizabeth Oming'o Kwa ajili ya kuwapatia watu wenye uhitaji katika Kituo Cha afya Cha Likombe.
Akizungumza baada ya kukabidhi vyandarua hivyo Leo Januari 2, 2025 Kituoni hapo, Mhe. Mtenga amemsisitiza Mganga Mfawidhi wa kituo hiko Dkt.Victor Andrea kuvigawa vyandarua kwa watu wenye uhitaji na kuisisitiza Idara ya afya kuweka mpango kazi na mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo kwa kuwahimiza wananchi kufanya usafi kwenye maeneo wanayoishi ili kuua mazalia ya mbu wanaosabisha ugonjwa wa malaria.
Katika hatua nyingine Mhe. Mtenga amewashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wa kituo cha afya cha Likombe Kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi hali inayopeleka wagonjwa kukimbilia kituoni hapo kufuata huduma bora.
Aidha amemuagiza Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Dkt. Elizabeth Oming’o kuweka dirisha la kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kukata bima ya afyankwenyenkila Kituo Cha afya na Zahanati na amewasisitiza wananchi kukata bima za afya ili waweze kupata matibabu ya uhakika
Ili kuimarisha usalama wa mazingira katika Kituo hiko, Mhe. Mtenga ameahidi kuchangia tofali 2000 na mifuko ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa uzio.
Kwa upande wake Mratibu wa malaria Manispaa ya Mtwara-Mikindani.... amesema kuwa kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria kimeongezeka kutoka asilimia 7.2 mwaka 2023 hadi asilimia 8.9 mwaka 2024 kwa sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi, uwepo wa mabwawa, madimbwi na vyanzo vingine vya maji pamoja na uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi.
Amesema kuwa ili kudhibiti ugonjwa huo Manispaa inaendelea kuhamasisha matumizi ya
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.