Baada ya kupokea fedha Shilingi milioni mia moja hamsini (150,000,000) kutoka Serikali Kuu kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Kituo cha afya cha Ufukoni kilichopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani kimetumia fedha hizo kununua vifaa tiba vya kisasa vikiwemo seti ya mashine ya kung’oa meno, Ultra sound, darubuni, pamoja na vifaa vingine ili kuboresha utolewaji wa huduma za afya katika kituo hiko.
Mganga Mfawidhi wa kituo hiko DR. Christa Nzali amesema kuwa uwepo wa vifaa tiba hivyo itasaidia kusogeza huduma karibu na wananchi wapatao elfu ishirini ambao wanakadiriwa kupata huduma katika kituo cha afya cha Ufukoni kila mwaka.
Ametaja faida nyingine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ya Kituo kutokana na kuongezeka kwa huduma ambazo awali zilikuwa hazitolewi pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa kutoka wagonjwa 2000 kila mwezi hadi wagonjwa 3000.
Aidha Dkt. Nzali ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kukipatia kituo hiko fedha za ununuzi wa vifaa tiba pamoja na fedha nyingine Shilingi bilioni moja (1,000,000) zilizotumika kuboresha miundombinu ya afya ikiwemo ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (0PD), maabara, wodi ya mama na mtoto, jengo la upasuaji, njia z watembea kwa miguu pamoja na jengo la kufulia nguo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.