Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig. Jen Marco Gaguti ametoa agizo la kivuko MV Mafanikio kinachofanya safari zake kuanzia Feri hadi Msangamkuu kuwa kuanzia Oktoba 4, 2021 Kivuko hiko kitahudumia wananchi hadi saa mbili usiku badala ya saa 12 jioni ili kuruhusu wananchi hao kupata muda zaidi katika shughuli zao za kila siku.
“Kumekuwa na changamoto ya suala la muda na mmeomba muda uongezwe, tumeridhia kivuko hiki sasa kifanye kazi mpaka saa mbili usiku”Amesema Gaguti
Mhe. Gaguti ametoa agizo hilo Oktoba 4, 2021 wakati wa mapokezi ya kivuko cha MV. Mafanikio kilipowasili Mkoani Mtwara baada ya kufanyiwa ukarabati ambao umegharimu kiasi cha shilingi Mil 493,609,357.70.
Aidha amewataka wananchi hao kuhakikisha wanalipa kodi kwa usahihi na wakati ili Serikali iweze kuwekeza na kuleta miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Mtwara.
“Tujitahidi kulipa kodi hii miradi inayoendelea kutekelezwa katika Mkoa wetu inahitaji uwekezaji wa kutosha, kodi zetu zina tija katika kuleta maendeleo” Amesema Gaguti
Naye Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mkoa wa Mtwara Eng. Japhet Msellu amesema kuwa kivuko hicho kimefanyiwa ukarabati wa injini na baadhi ya vifaa ambapo matengenezo yote yamegharimu kiasi cha shilingi Milioni 493,609,357.70 pamoja na ongezeko la VAT.
Nae Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassani Mtenga amewataka wananchi kutofanya uharibifu katika miundombinu ya kivuko hicho kwani uharibifu huo utakwamisha shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.
Bakari Omari Ally mkazi wa Msanga Mkuu ameishukuru Serikali kwaajili ya ukarabati huo kwani kina usalama zaidi katika matumizi tofauti na mitubwi ambayo inatumika kwa sasa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.