Kamati ya Mipangomiji Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Leo Tarehe 17 Januari 2025, imefanya ziara ya kutembelea miradi miwili inayohusisha kamati hiyo,inayoendelea kutekelzwa ndani ya Halamshauri.
Ikiongozwa na Diwani wa Kata ya Naliendele Mhe.Masudi Dali ,kamati imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Mipangomiji iliyopo mtaa wa Rahaleo Juu, kata ya Rahaleo ndani ya Manispaa ambayo ujenzi wake umekamilika kwa kiasi kikubwa.
Aidha Kamati imetembelea kiwanja namba 407 ambacho ,Manispaa imepokea maombi ya kubadilisha matumizi ya kiwanja hicho kutoka matumizi ya sasa (Ukumbi wa Sinema) kuwa kituo cha mafuta (Petro Station)
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.