Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) ya Wilaya ya Mtwara, leo tarehe 21 Mei, 2025 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyochaguliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa ajili ya kukaguliwa, kuwekewa jiwe la msingi na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru hapo Jumapili (25/05/2025).
Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mtwara, Mhe. Abdalah Mwaipaya, wametoa maboresho madogo katika miradi inayohitaji kuboreshwa zaidi pia wamepongeza juhudi na jitihada za Manispaa kwenye uchaguzi wa miradi.
Katika siku husika Mwenge wa Uhuru Utapokelewa katika eneo la Soko la Milumba na Mkesha utakuwa katika Viwanja vya Sabababa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.