Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko kuendelea kukusanya mapato katika Soko la Sabasaba wakati taratibu za kimahakama kuhusiana na mgogoro kati ya soko la sabasaba na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani zikiendelea.
Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo leo Mei 7,2021 alipozungumza na wafanya biashara wa soko la Sabasaba kilichofanyika katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
“ Nimesikia kuna watu wanazuia ukusanywaji wa kodi, nakuagiza Mkurugenzi taratibu za Halmashauri ziendelee kama kawaida, kodi iendelee kukusanywa , kama kuna mtu ana malalamiko yoyote afate taratibu atasikilizwa , mtu akizuia ukusanywaji wa kodi tutamshughulikia”
Makusanyo ya kodi ndio yanayoendesha shughuli katika Manispaa yetu, sasa anatokea mtu mmoja au kikundi kinashawishi wafanya biashara wasilipe kodi, haitawezekana ,sitaweza kuona maendeleo ya Manispaa hii yanakwamishwa na watu wachache”amesema Kyobya
Aidha amewataka wafanyabiashara hao kuendeleza vizimba vyao vya biashara vilivyopo katika soko la Chuno, kushindwa kufanya hivyo kutamlazimu Mkurugenzi kugawa vizimba hivyo kwa wafanya biashara wengine ambao wamekosa vizimba katika Soko hilo ili waweze kuendeleza biashara zao.
Mwisho amewataka wafanyabiashara hao kushirikiana katika kulinda usalama wa raia kwa kuepuka kutoa ushawishi wa ugomvi na visasi baina yao na kutoa taarifa kwa vyombo husika pindi wanapoona kuna uvunjifu wa amani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.