Mratibu wa Usajili wa Utoaji wa Vyeti vya Kuzaliwa Kwa Watoto Wenye Umri Chini ya Miaka Mitano Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Felista Kyando, amewataka akina mama kuacha tabia ovu ya kubadilisha jina la mzazi wa kiume (baba) wa mtoto, kwenye cheti cha kuzaliwa cha mtoto wao pale inapotokea migogoro baina yao kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na inamnyima haki mtoto.
Kyando ameyasema hayo Leo Mei 15,2025 kwenye maadhimisho ya siku ya familia Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo katika Manispaa hiyo na kuwakutanisha wazazi ,walezi na wanafunzi wa vituo vya malezi ya Watoto mchana.
Aidha amewahimiza wazazi kuandaa majina ya watoto wao mapema pindi mama anapokuwa mjazito ili mtoto anapozaliwa aweze kusajiliwa na kupatiwa cheti cha kuzaliwa kabla mama hajatoka hospitali na kuondoa usumbufu wa kufuatilia cheti hiko.
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Manispaa hiyo Bwana. Emanueli Moshi amewataka wazazi hao kuhakikisha wanawapatia lishe bora watoto wanapokuwa nyumbani ili waweze kukua vizuri.
Nae Mratibu wa Chanjo Bwana. Nelson Maro amesema kuwa chanjo zote zinazotolewa na Serikali ni salama hivyo amewaomba wazazi kuwapeleka watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwenye vituo vya kutolea huduma kwa ajili ya kupata chanjo ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali kama ya kupooza na magonjwa mengine.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.