Katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini, Benki ya NMB Kanda ya Kusini imekabidhi viti mwendo vitano (WHEEL CHAIR) Pamoja na vitanda viwili vya kujifungulia (Delivery beds) kwa akina mama wajazito vyenye thamani ya shilingi milioni tano (5,000,000) Katika Kituo cha afya Likombe kilichopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Akizungumza mara baada ya Kupokea vifaa hivyo Mei 23, 2022 Afisa Tarafa ya Mtwara Mjini ambae pia alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Ndugu Saidi Kayangu ameipongeza Benki hiyo kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kuleta Maendeleo hapa nchini.
“Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inatambua mchango wa NMB, inatambua namna benki inavyoshirikiana kikamilifu na serikali na namna inavyomuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuleta maendeleo” amesema Kayangu
Aidha Kayangu amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani na baraza la Madiwani kwa kuona umuhimu wa kusukuma maendeleo mbele na kutekeleza miradi inayoboresha sekta ya afya.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada walioutoa kwani imeipunguzia mzigo Manispaa kwa kuwa fedha ambazo zingetumika kununua vifaa hivyo itasaidia kutekeleza miradi mingine ya Maendeleo.
Kwa upande wake Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Kusini Bi. Janeth Shango Benki hiyo inatambua Juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita na kwamba wana wajibu wa kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha inatumia faida wanayoipata kutoa misaada katika jamii hasa katika sekta ya afya na elimu.
Amesema kuwa Benki hiyo imejiwekea utaratibu wa kuendelea kutoa misaada kwa jamii na kwa mwakae huu imetnga shilingi Bilioni 2 kusaidia katika sekta hizo.
Bi. Agness Kalanje mkazi wa Matopeni ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada walioutoa kwani itasaidia kupunguza foleni kwenye utoaji wa huduma kwa akina mama wanaojifungua na hospitali itaweza kuhudumia idadi kubwa ya akina mama hao kwa wakati mmoja.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.