Katika kuazimisha siku ya wauguzi duniani ifikapo tarehe 12 Mei , Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Halmashauri ya Mtwara Mikindani Bi. Tamko M. Ally ametoa rai kwa wauguzi wa kituo cha Afya cha Likombe na Mikindani , kufanya kazi kwa ufanisi na uaminifu katika kuboresha utoaji wa huduma ya afya ili kutomeza vifo vya mama na mtoto kabla na baada ya kujifungua.
“ Tunatamani kuona mama anapokuja na tumaini la kupata mtoto tumaini hilo isiishie leba mama huyo arudi na mtoto nyumbani kwake, hii yote itafanikiwa kama nyie wauguzi,madaktari na wahudumu wengine wa afya mtafanya kazi zenu kwa ufanisi katika kitengo hiki cha uzazi” Alisema
Bi. Tamko alitoa rai hiyo tarehe 12 Mei alipozungumza na wauguzi wa kituo cha afya cha Likombe na Mikindani waliposheherekea siku hiyo ikiwa ni sehemu moja wapo ya kutambua kazi kubwa inayofanywa na wauguzi hao.
Aliongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu na mchango wa wahudumu wa afya katika kutokomeza vifo vya mama na mtoto, hivyo wametakiwa kuendelea kutimiza majukumu yao ya kila siku kwa uaminifu na ufanisi katika kuboresha utoaji wa huduma ya afya.
‘’ Tunatambua bidii yenu katika kuokoa maisha ya mama na motto, nataka niwahaikishie Serikali inatambua jitihada zenu, naomba muuendelee kuchapa kazi kwa upendo na uaminifu” Alisema Bi. Tamko
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.