Maafisa waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo wametakiwa kufanya kazi ya Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa weledi ,bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hilo la Kitaifa.
Wito huo umetolewa na Afisa mwandikishaji wa Jimbo La Mtwara Mjini George Mbogo kwenye hotuba yake akiwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya Uboreshaji wa Daftrai hilo iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Mtwara Kawaida.
“Kwa kutumia uzoefu huo wa mafunzo mtakayopatiwa, natarajia mtafanya kazi kwa weledi, bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hili la Kitaifa “Alisema
Akaongeza “Ni matumaini yangu kuwa kutokana na semina hii kila mmoja wenu atapata elimu ya kutosha itakayomwezesha kutekeleza majukumu yake ili kufanikisha zoezi hili’
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.