Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na miongozo itakayotolewa na Tume ya Uchaguzi ili kufanikisha malengo tarajiwa ya kuboresha Daftari la kudumu la wapiga kura.
Maagizo hayo yametolewa na Afisa Mwandikishaji Msaidizi Jimbo la Mtwara Mjini, Juliana Manyama wakati wa kufunga Semina ya mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Mtwara (K).
Alisema ni vema Maafisa hao kutambua kwamba wamebeba dhamana kubwa na maelekezo waliyopewa ni zana ya kuwawezesha kutekeleza kwa ufanisi majukumu yao.
Aidha, aliwahimiza Maafisa hao kuwahamasisha wananchi wenye sifa wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi.
"Jukumu la uhamasishaji linawahusu moja kwa moja ninyi Watendaji, kwa kushirikiana na wadau wengine katika maeneo yenu," alisema.
Kwa upande wake, Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mtwara Mjini, George Mbogo aliwataka Maafisa hao kutosita kuwasiliana na Tume kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala yote yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu yao.
"Tume imeteleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na hivyo nanyi mna wajibu wa kuhakikisha kuwa mnatekeleza kikamilifu kwa upande wenu," alisisitiza Mbogo.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa upande wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani litaanza tarehe 28 Januari na kutamatika tarehe 03 Februari 2025.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.