Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amefurahishwa na namna madarsa yanayoongea yalivyoandaliwa na walimu na wanafunzi kama dhana ya kufundishia na ubunifu wa kitaaluma kwa lengo la kuonesha namna ambavyo mwalimu anaweza kutumia vifaa katika kuwezesha ufundishaji wa stadi za kusoma , kuandika na kuhesabu kwa darasa la kwanza na la pili Pamoja na masomo ya sayansi na hisabati.
Mhe. Kyobya amewataka walimu kuendeleza madarsa hayo kwenye shule zao hata baada ya Juma la Elimu kumalizika ili kumfundisha mwanafunzi kwa vitendo
Maonesho hayo yamefanyika leo Machi 28, 2022 kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yaliyofanyika Shule ya Msingi ya Majengo
Katika Ukaguzi huo Mhe. Mkuu wa Wilaya pia aliambatana na Naibu meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Saidi Ally Nassoro Pamoja na wageni wengine wakiwemo Madiwani wa Kata za Tandika na Majengo, Maafis aElimu Pamoja na wadau wengine wa Elimu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.