Ili kupunguza changamoto za wananchi kwenye kata zilizopo, Mstahiki meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani amewataka Madiwani kuanza kubuni na kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao kwa kuwashirikisha wananchi ili manispaa na Serikali Kuu ziweze kuunga mkono jitihada hizo.
Amesema kuwa sambamba na Serikali kuleta fedha za miradi mbalimbali amewataka madiwani hao kuhamasisha wananchi kujitolea nguvu kazi kwa kuwa Serikali inatambua uhitaji wa wananchi kupitia juhudi zao katika kujitolea kwenye kuanzisha miradi.
Aidha Mhe. Ndile amemuagiza Mkurugenzi kuzingatia muda uliotengwa katika kukamilisha miradi, ubora ili thamani ya fedha ionekane.
Hayo yamesemwa Mei 25,2023 katika mkutano wa baraza la madiwani wa kupitia na kujadili taariza za Kata uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Ualimu kawaida Kilichopo Manispaaya Mtwara-Mikindani
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.