Wakati Mkoa wa Mtwara ukijiandaa kuwasha Mwenge wa Uhuru Kitaifa April 2, 2023 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani Shadida amewaongoza waheshimiwa Madowani na Timu ya Menejimenti kufanya ziara ya ukaguzi w amiradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru April 2, 2023.
Lengo la kufanya ziara hiyo ni kukagu ana kuona maendeleo ya utekelzaji wa miradi itakayopitiwa na mwenge huo.
Aidha waheshimiwa madiwani wameridhika n ahatua za utekelzaji wa miradi hiyo na kuwataka wataalamu na wakandarasi kuhakikisha wanaharakisha ujenzi wa miradi ili iweze kukamilika kwa wakati na kwa kuzingatia ubora wa miradi uliowekwa.
Miradi inayotarajiwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru ni Pamoja na ujenzi wa barabara ya Mitengo hospitali ya Kanda y aKusini km 1 kwa kiwango ch alami, ujenzi wa tenki la kusambaza maji Mtawanya, ujenzi wa madarasa matatu na ofisi Shule ya Sekondari yaa shangani, kukagua shughuli za ubanguaji wa korosho kiwanda cha coastal Nuts Reli Pamoja na kiwanda cha kutengeneza bidaa za ngano Mangamba.
Mirdai mingine ni pamoa ja na ujenzi wa jingo la upasuaji, ,wodi ya mama na mtoto na jingo la kufulia Kituo ch aafya Ufukoni.
Mtwara-Mikindani tumejiandaa kuwasha na kuzindua Mwenge 2023.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.