Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile amewataka Madiwani wa Manispaa hii kuhakikisha wanatumia vizuri mitandao ya kijamii katika kuwapa majibu wananchi penye sintofahamu ili kuondoa taharuki kwa wananchi hao.
“Diwani mzuri ni yule anayetafuta majibu ya serikali na kuwajibu wananchi, diwani ni mtu wa kutoa majibu na sio kuleta taharuki kwenye jamii, tuzingatie hilo kwa maslahi mapana ya Halmashauri yetu”amesisitiza Mhe Ndile
Mstahiki Meya ameyasema hayo April 30, 2022 kwenye mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Shule ya sekondari ya Call and Vision iliyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Aidha Mhe. Ndile amewataka madiwani na wataalamu kuwa waadilifu kwenye miradi yote inayoendelea kutekelezwa ili iwe mizuri na iweze kutumika kwa muda mrefu .
Mhe. Ndile pia ametoa wito kwa wananchi wote wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuhakikisha wanadumisha usafi katika mji wetu na kulipa ada ya uzoaji wa taka ngumu ili Manispaa iweze kutoa hudum ya uzoaji w ataka kwa ufanisi .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.