Ikiwa leo Mei 28, 2023 ni siku ya hedhi salama, Madiwani wa viti maalumu Manispaa ya Mtwara-Mikindani wameungana kutoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wasichana wenye mahitaji maalumu (wenye ulemavu wa akili) wanaosoma Shule ya Msingi Shangani .
Pamoja na taulo za kike madiwani hao pia wamekabidhi juisi na biscuit kwa wanafunzi wote wa kike na wa kiume ikiwa ni sehemu ya kufurahi nao pamoja.
Madiwani hao wamesema kuwa wameamua kutumia siku hiyo kugawa taulo za kike na vifaa vingine kwa wanafunzi hao ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanasoma kwenye mazingira bora kama walivyo wanafunzi wengine.
Aidha walitumia muda huo kuwafundisha wanafunzi hao namna ya kuzitumia taulo hizo za kike na jinsi ya kuzihifadhi mara baada ya kuzitumia huku wakiwasisitiza kuwa wasafi muda wote..
Kwa upande wake Mratibu wa Elimu Kata Sister orester Nyakolema amewashukuru viongozi hao kwa jinsi walivyotoa kuwasaidia wanafunzi hao na amewaomba wadau wengienwa maendeleo waliopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani kujitoa kuwasaidia wanafunzi hao kw akuwa wana mahitaji mengi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.