Wakati zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura likiendelea Mkoani Mtwara, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Gwakisa Mwasyeba amewaomba Wajumbe wa Baraza la Madiwani Kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao na kuwahamasisha wananchi wao kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari hilo.
Aidha Mwasyeba amewaomba Wajumbe hao kuwahimiza wananchi kuwapeleka watoto shule na Kuhakikisha hakuna mtoto hata mmoja anabaki nyumbani .
Ameyasema hayo leo Januari 30,2025 kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili na Kupitia Taarifa ya robo ya pili ya kujadili na Kupitia Taarifa za Kata uliofanyika Katika Ukumbi mdogo wa shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.