Baada ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kutoa zaidi ya Shilingi milioni 209 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo na shughuli nyingine kwa kutumia fedha za mapato ya ndani katika robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Shadida Ndile amewataka Madiwani kuendelea kusimamia na kukusanya mapato pamoja na kutoa elimu na mrejesho kwa wananchi wa matumizi ya kodi zao kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili changamoto zilizopo Kwenye Kata na Mitaa ziweze kutatuliwa.
Mstahiki Meya ameyasema hayo Leo Novemba 7,2024 kwenye Mkutano wa baraza la Madiwani wa kujadili na kupitia taarifa za za utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwenye Kata , uliofanyika katika Ukumbi wa Manispaa.
Aidha amewahimiza Madiwani hao kupeleka vipaumbele viliyopo kwenye Kata kwa Mkurugenzi ili aweze kuvifanyia kazi huku akiahidi kubaini miundombinu yote chakavu ya shule ili iweze kurekebebishwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani na zile zinazotoka Serikali Kuu.
Amesema kuwa halmashauri itaendelea kuboresha miundmbinu ya masoko yote awamu kwa awamu ambapo kwa awamu ya kwanza halmashauri imepeleka Shilingi milioni 10 Kata ya Vigaeni kwa ajili ya kuboresha soko Kuu eneo la Mkunguni.
Ameendelea kulitumia baraza hilo kuipongeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani hususani sekta ya elimu kwa kuongoza Kimkoa kwenye matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka huu ambapo Manispaa imefaulisha kwa daraja A,B na C.
Kwa nyakati tofauti Waheshimiwa Madiwani wamepongeza Mstahiki Meya, Mkurugenzi Mwalimu Nyange na wataalamu wake kwa kutoa fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezji wa miradi ya amendeleo na shughuli nyingine kwenye Kata .
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara Ndugu Mwinyi Ahmed Mwinyi amewataka wajumbe wa baraza hilo kujiandaa vizuri na uchaguzi wa Serikali za mitaa
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.