Kupitia MKutano wa baraza la Madiwani wa kujadili na kupitia taarifa mbalimbali za Kata uliofanyika Oktoba 28,2021 Katika Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Kawaida (TTC), Wajumbe wa Mkutano huo wameishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 shilingi 440,000,000 zitakazotumika kujenga madarasa ishirini na mbili ya Shule za Sekondari.
Akizungumza kuhusu fedha hizo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Shadida Ndile amewataka Madiwani kusimamia miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwahamasisha wananchi ili waweze kujitokeza kuchangia nguvu kazi pindi miradi hiyo itakapoanza.
Katika hatua nyingine Madiwani hao wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuchochea maendeleo katika Wilaya yetu ikiwemo utatuzi wa Migogoro mbalimbali.
Aidha wamempongeza Mkurugenzi wa Manispaa Col. Emanuel Mwaigoibeko na timu ya wataalamu kwa kusimamia miradi kwa ufanisi.
Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuanzia mwezi Januari mwaka huu hadi sasa tumepokea shilingi Bilioni. 1,257,134, 139.58 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Miundombinu mbalimbali ya shule na Zahanati hakika tuna haki ya kuishukuru Serikali kwa kutuona.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.