Katika Kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yaliyopo sasa ,Manispaa ya Mtwara-Mikindani imekabidhi vishkwambi 50 vyenye thamani ya Shilingi 32,155,000 kwa waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo ili kuwezesha ufanisi wa Utendaji kazi katika vikao mbalimbali vya kisheria pamoja na kupunguza gharama ya ununuzi wa shajala zinazotumika katika maandalizi ya makblasha yanayotumika Kwenye vikao hivyo.
Vishkwambi hivyo vimekabidhiwa Leo Novemba 8, Kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za Halmashauri robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025 uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa hiyo.
Akizungumza mara baada ya Kukabidhi vifaa hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe.Shadida Ndile amewaasa waheshimiwa Madiwani na Wataalamu hao kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na kuvitunza ili viweze kudumu Kwa muda mrefu.
"Sitarajii kuona mnatumia vibaya vishkwambi hivi, Wala kuvitumia Kwa matumizi binafsi,na atakaebainika kuvitumia vifaa hivyo kuvujisha Siri za Serikali atachukuliwa hatua za kisheria"amesisitiza Mhe.Ndile.
Awali akisoma taarifa ya ugawaji wa vifaa hivyo ,Mkuu wa Kitengo Cha TEHAMA Manispaa ya Mtwara-Mikindani Athumani Mfaume amesema kuwa vifaa hivyo vimenunuliwa Kwa ajili ya kupokea na kutunza taarifa za Serikali ambazo ni Siri na mtu yeyote hataruhusiwa kusambaza kwa mtu yeyote pamoja na mitandao ya kijamii.
Amesema kuwa vifaa hivyo havitatumika katika mazingira hatarishi ambayo yatapelekea
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.