Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyosaidia kutatua kero mbalimbali za wananchi kwenye Kata.
Waheshimiwa madiwani wametoa shukrani hizo Leo Januari 30, 2023 kwenye mkutano wa baraza la Madiwani la uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizofanyika kwenye Kata katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mtwara-Ufundi
Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Kuanzia Julai 2022 hadi sasa imepokea fedha shilingi Bilioni moja milioni mia tano arobaini laki mbili themanini na sita mia tatu tisini na tatu na senti sabini na saba (1,540,286393.77) kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya Mjimwema ( 500,000,000), ununuzi wa gari la kubeba wagonjwa (174,036,393.77), ununuzi wa vifaa tiba Kituo cha afya Ufukoni (150,000,000) na zahanati ya Mbawala Chini (50,000,000) ujenzi wa madarasa ishirini na moja ya Sekondari (420,000,000).
Miradi mingine ni Pamoja na umaliziaji wa bweni la Shule ya Sekondari ya Naliendele (40,000,000), ukarabati wa nyumba vya madarasa ya Shule za Msingi (156,250,000) Pamoja na umaliziaji wa Zahanati ya magomeni (50,000,000).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.