Baada ya Wajumbe wa baraza la Madiwani kuwasilisha changamoto mbalimbali zilizopo kwenye kata zao , Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewasisitiza Madiwani kuwa hao wabunifu kwa kuwashirikisha Wadau mbalimbali wa Maendeleo ili waweze kuchangia shughuli za Maendeleo katani.
Mkuu wa wilaya amesema hayo Julai 27, 2022 kwenye Mkutano wa baraza la Madiwani la uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwenye kata lililofanyika katka Ukumbi waChuo cha Ualimu kawaida.
Aidha Mhe. Kyobya awewataka madiwani hao kuyasema mambo mazuri yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita kwenye Mikutano ya Kata kwa kuwa Miradi mingi imetekelezwa.
Kutokana na uwepo wa Sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika Agosti 23, mwaka huu, Mkuu wa wilaya amewataka madiwani kutumia nafasi zao katika kuhamasisha zoezi hilo.
“Sijaridhika na kasi ya hamasa ya Sensa ya watu na makazi katika nagzin ya kata , nichukue nafasi hii kuwaomba mkaitishe mikutano huku tukiwaahusisha viongozi wa dini na taasisi zote zilizopo kwenye kila kata “ amesema Mhe. Mkuu wa wilaya.
Mkuu wa wilaya pia amesisitiza usimamiaji wa usafi wa mazingira kwenye maeneo yote Pamoja na upandaji wa miti huku akiwataka wajumbe kusimamia ulinzi na Usalama katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile amesema kuwa ameyapokea maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa wilaya na kuwasisitiza wajumbe wa baraza kila mmoja kwa nafasi yake akatekeleze maagizo hayo.
Aidha amevishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha kuwa kazi mbalimbali za wananchi zinafanyika katika hali ya usalama na utulivu
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.