Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mhe Evod Mmanda amelipongeza baraza la madiwani pamoja na timu ya wataalamu kwa kazi nzuri wanayoifanya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Amesema kuwa miradi mingi inayotekelezwa ndani ya Manaispaa imeonesha imetekelzwa kwa kiwango kizuri na thamani ya fedha inaonekana hata kwa mtu ambae hana utaalamu katika sekta ya Ujenzi.
Mmanda amezungumza hayo Mei 3, mwaka huu kwenye kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa na kuitaka Manispaa kuweka mkakati wa kuhakikisha inaongeza mapato ili kutekeleza miradi mingi Zaidi.
“Kazeni buti katika kuongeza vyanzo vya mapato, panueni wigo wa mapato, kusanyeni mapato kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na kwa ubinaadamu”alisema Mmanda
Kwa upande mwingine viongozi wa vyama vya siasa walialikwa kwenye baraza hilo hawakusita kutoa pongezi zao kwa menejiment ya manispaa inayoongozwa na Mkurugenzi kwa ukusanyaji mzuri wa mapato pamoja na utekelezaji na usimamizi wa miradi ya Maendeleo
“bila kuangalia itikadi ya vyama nampongeza Mkurugenzi tunaona mambo yanafanyika haki yake apewe, anafanya kazi” alisema Saidi kulagha Katibu CUF Wilaya
Nae Hassan Mbangile Katibu CHADEMA Wilaya amepongeza Mkurugenzi kwa kusimamia miradi na kuwataka wajumbe baraza la Madiwani kusimamia miradi hiyo..
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe.Geofrey Mwanichisye amesema kuwa ataendelea kusimamia Manispaa bila ya kuelemea upande wowote na kwamba amepokea mawazo na ushauri kutoka pande zote kwa kuwa kwenye Maendeleo hakuna upinzani kwani Maendeleo hayana vyama
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani bi Beatrice Dominic ameshukuru kwa pongezi zilizotolewa na kuahidi kuendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za Manispaa kwa kufuata miongozo iliyowekwa.
Amesema kuwa katika bajeti ya 2017/2018 hadi kufikia robo ya tatu imetumia kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kutekeleza miradi ya Maendeleo kutoka katika mapato yake ya ndani na fedha hiyo imekeleza miradi ya Maendeleo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.