Baada ya Madiwani kuwasilisha taarifa za uhaba wa miundombinu mbalimbali ya shule kwenye maeneo yao, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile amewataka Madiwani hao kuwahamasisha wananchi kwenye Kata zao ili waweze kuchangia katika sekta ya elimu kwa kuanzisha miradi ya Maendeleo ili Serikali iweze kuunga mkono jitihada za jamii.
Amesema kuwa kwa sasa Serikali imetoa muongozo unaosisitiza wananchi kuanzisha miradi na kuimalizia hivyo ni jukumu la Madiwani na watendaji kuanzisha miradi ya maendeleo kwenye Kata na Mitaa.
Mstahiki Meya ameyasema hayo Januari 26,2022 kwenye kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi katika Ukumbi wa Chuo Cha ualimu Kawaida kwa ajili ya kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Kata.
Aidha Mstahiki Meya amewataka Madiwani na watendaji kufanya kazi kwa kushirikiana ili Manispaa yetu iweze kusonga mbele
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.