Baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuwa na mahakama ya mwanzo Katika Kata ya Mtawanya na kupelekea wananchi kutembea umbali mrefu kwenda mTwara Mjini kupata huduma za kimahakama , hatimae leo Juni 29,2021 Jaji Mfawidhi wa mAhakama kuu Kanda ya Kusini Mhe.Joel Paul Ngwembe amefungua huduma za kimahakama zitakazotolewa kila siku Katika ofisi ya Kata ya Mtawanya na kuwomba wananchi kutoa ushirikiano kwa watumishi watakaofanya kazi katika mahakama hiyo.
Mhe. Ngwembe amesema kuwa ofis yake imemua kuanzisha huduma hiyo ili kuwasogezea wananchin huduma kwa ukaribu na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.
Kutokana na uwepo wa huduma za kimahakama katika eneo hilo Jaji amewataka wananchi wa Mtawanya kutojichukulia sharia mkononi na kugomban hovyo katika maeneo yao badala yake waitumie kupata Suluhu ya matatizo yao bure.
“Ufunguaji wa mashauri hauna gharama, unaweza kufungua kwa njia ya mtandao, hakuna sababu ya kugomban hovyo mtaani, vipo vyombo vilivyofundishwa kwaajili ya kutatua matatizo yenu” Alisema Ngwembe
Aidha amewaomba wananchi hao kutumia hakimu aliyepangiwa kituo vizuri katika kutatua mogogoro yao ya kila siku.
Kwa uapnde wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Dunstan Kyobya amewashukuru Jaji Ngwembe kwa kurudisha mahakama ya mwanzo Mtawanya kwani ni kiu ya muda mrefu ya wananchi wa eneo hilo.
Nae Diwani wa Kata ya Mtawanya Mhe. Ahmad Kalikumbe amesema kuwa amefurahi sana kuona Mahakama ya mwanzo inarejeshwa tena katika Kata yake na kwamba uwepo kwa hakima mwanamke katika mahakama hiyo ana Imani haki itatendeka.
Huduma za Mahakama ya mwanzo Mtawanya zinaanza kutolewa Juni.30,2021 na tayari hakimu wa Mahakam hiyo ameshateuliwa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.