Kama ilivyo kwenye halmashauri nyingine nchini Tanzania Manispaa ya Mtwara-Mikindani imesaini makubaliano (memorandum of understanding) na mji wa suquian uliopo nchini China juu ya uimarishaji wa uhusiano kati ya miji hiyo miwili.
Makubaliano hayo ambayo yamefanyika oktoba 16, 2018 kwenye ofisi ndogo ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na kushuhudiwa na mhe. Gelasius Byakanwa Mkuu wa Mkoa pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa,yamelenga kuimarisha uhusiano na kushirikiana katika maeneo mbalimbali.
Meya wa mji wa suqian Ye hui ameyataja baadhi ya maeneo ambayo wangependa kufanyia uwekezaji kuwa ni pamoja na maeneo ya elimu, kilimo, michezo, utamaduni na utalii pamoja na Uvuvi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amewakaribisha wageni hao na kuwataka kuwekeza Mtwara kwa kuwa zipo fursa nyingi ikiwemo uwepo maeneo ya kupumzikia (beach)nzuri, uwepo wa mji wa kitalii mikindani n.k
Aidha Kabla ya kusaini kwa makubaliano hayo Manispaa ya Mtwara Mikindani iliwasilisha mbele ya wageni maeneo ya uwekezaji yaliyotengwa hasa maneno ya viwanda ili kuwavutia wageni hao waweze kuwekeza ndani ya Manispaa ya Mtwara -Mikindani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.