Baada ya kusubiri kwa muda hatimaye, ukarabati wa Soko la Kiyangu lililopo Mtaa wa Kiyangu A, Kata ya Shangani kuanza rasmi hivi karibuni.
Hatua hii muhimu imefikiwa mara baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange, kukutana na Wafanyabiashara wa soko hilo ili kujadili njia bora za uboreshaji wa mazingira ya biashara sokoni hapo.
Akiwa ameambatana na Diwani wa Kata ya Shangani, Mheshimiwa Abuu Mohamed, Mkurugenzi alieleza kwamba zoezi hili litahusisha kuvunjwa kwa vibanda vilivyopo na kujengwa 'shedi' za kisasa katika soko hilo, kuhakikisha mazingira ya biashara yanakuwa ya kisasa zaidi.
Aidha, alisisitiza kwamba wakati wa kipindi cha ukarabati, wafanyabiashara 6 wanaofanya biashara eneo hilo watalipwa fidia ya Tsh. 12,000 kwa siku kwa kipindi cha mwezi mmoja, ili kusaidia kupunguza athari za biashara zao.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Abuu, mbali na kumpongeza Mkurugenzi, aliwakumbusha wafanyabiashara kuwa suala la biashara ni mtambuka, akisisitiza kuwa biashara si kuuza bidhaa pekee bali yanatakiwa mazingira rafiki ya kufanya biashara husika.
Vilevile, ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kutoa ushirikiano wa karibu katika kipindi chote, kwani maboresho haya yana manufaa makubwa kwao na kwa jamii kwa ujumla.
#tunatekeleza
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.