Mamia ya wananchi kutoka kata mbalimbali zilizopo Tarafa ya Mikindani wamejitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi wa tamasha la michezo ya asili (bao na draft) lijulikanalo kama “MTONYA FESTIVAL” lililoandaliwa na diwani wa Kata hiyo, Mhe. Shadida Ndile (Mstahiki meya wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikidani) Leo Septemba 20 katika Viwanja vya Ofisi ya Kata hiyo.
Mhe. Ndile amesema kuwa ameanzisha tamasha hilo ili kutimiza nia yake ya kuendeleza sekta ya michezo ndani ya Manispaa na kuleta furaha kwa wanajamii mara baada ya shughuli ya kutwa nzima ya kujitafutia kipato huku akiamini kuwa michezo inaimarisha afya na inaleta ajira Manispaa pamoja na kuhabarishana juu ya uwepo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024 hapa nchini.
Ameendelea kusema kuwa katika tamasha hilo amehusisha timu nane za bao na draft na amewashukuru wachezaji kwa kulipokea wazo lake ambapo
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.