Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kuwa na mikakati na usimamizi mzuri wa mapato yake, jinsi inavyoendesha minada ya samaki sanjari na kuchangamkia fursa ya uwekezaji wa Mazao ya Baharini.
Hayo yamejiri leo (11/04/2025) ambapo Manispaa ya Kigamboni imeitembelea Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Ukusanyaji Mapato na usimamizi wa Sekta ya uvuvi na mazao ya baharini.
Wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Selemani Kateti na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Mhe. Ernest Mafimbo, wameipongeza Mtwara-Mikindani kwani wamejifunza mengi kuanzia kwenye Fursa za Mazao ya Baharini kama Ufugaji wa viumbe bahari ( Majongoo Bahari na Kaa) sanjari na uchakataji wa zao la mwani kutengenea bidhaa kama Sabuni, Mafuta, chakula dawa, nakadhalika.
Ukiwa umeambatana na Mwenyeji wao Naibu Meya, Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Mhe. Sixmund Lungu, Ugeni huo umetembelea maeneo kadhaa ikiwemo Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) – Kampasi ya Mikindani, pamoja na Soko la Samaki Feri.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.