Katika kuhakikisha kuwa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani inaendelea kukusanya mapato ili iweze kutekeleza miradi ya maendeleo , Timu ya Menejimenti imeanza operesheni maalumu ya ukaguzi wa leseni za biashara na kodi za mabanada ya baishara kwa wafanyabaishara wanaofanya biashara zao eneo la soko kuu.
Operesheni hii imeanza Mei 31,2022 na itendelea kwenye maeneo mengine ikiwemo stendi ya zamani ya mabasi , stendi ya Chipuputa , Soko la Kiyangu pamoja na maeneo mengine.
Tunaendelea kluwakumbusha wafanyabaishara wote waliopanga mabanda ya baishara ya Manispaa kuhakikisha wanalipa kodi za mabanda nakukata leseni za biashara ili kuondoa usumbufu.
Kumbuka kuwa kufanya baishara bila ya kuwa na leseni ya baishara ni kosa kisheria na adhabu yake ni faini ya shilingi laki mbili
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.