Walimu wakuu wa Shule za Sekondari tano za Manispaa ya Mtwara-Mikindani Julai 23,2018 wamepokea vyeti vya pongezi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa baada ya kufaulisha kwa asilimia 100 kwenye matokeo ya mitihani cha kidato cha sita 2018 yaliyotangazwa na baraza la mitihani hivi karibuni.
Jumla ya shule tano za Sekondari zenye kidato cha tano na sita zenye wanafunzi wapatao 642 wamefanya mtihani na kati ya hao, wanafunzi 60 wamefaulu kwa daraja la I, 294 wamefaulu kwa daraja la II, 281 daraja la III na wanafunzi 7 wamepata daraja la IV na kufanya ufaulu kuwa wa asilimia 100.
Manispaa ya Mtwara-Mikindani imedhamiria kuendeleza ufaulu kwa asilimia 100 huku ikitembea na kauli mbiu iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara inayosema “Mtwara iz a zero free zone in form six examination, play your party”.
Kwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Shule ya sekondari ya Mtwara Ufundi imeshika nafasi ya kwanza kwa ufaulu kwa kupata GPA ya 2.7, Aquinas GPA ya 3.…..,Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara GPA ya 3.15, Amana GPA ya 3.18 na Ocean GPA ya 3.48
Mkoa wa Mtwara umeshika nafasi ya kwanza kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha sita 2018 ikiwa na jumla ya shule 11 zenye wanafunzi 1,499 waliofanya mtihani huo na kufaulu kwa asilimia 100.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.