Baada ya kukamilika kwa mawasilisho ya taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali mkoa wa Mtwara na uwasilishaji wa majibu ya hoja za ukaguzi ,Mhe.Gelasius Byakanwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameipongeza Manispaa ya Mtwara-Mtwara -Mikindani kwa kupata safi kwa mwaka wa fedha wa 2016 /2017.
Amesema kuwa uwepo hati safi kwenye halmashauri yoyote ile ni ishara tosha ya kuonesha kuwa sheria, taratibu na miongozo ya Serikali inafuatwa hivyo amewataka wataalamu kuendelea kusimamia miongozo ,sheria na taratibu ili kupunguza hoja zisizokuwa na msingi.
Byakanwa amezungumza hayo Julai 27,2018 kwenye baraza maalumu la madiwani lililojadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa boma Mkoa.
Pamoja na pongezi hizo ameitaka Manispaa kuishirikisha ofisi ya mkaguzi wa hesabu za Serikali inapotaka kufanya manunuzi makubwa lakini pia kufanya kazi na makampuni yanayotoa risisti za EFD ili kuepusha hoja zisizo na ulazima ,
Aidha amempongeza mkurugenzi wa Manispaa na kumtaka kuongeza nguvu kwenye ukusanyaji wa mapato ili miradi ya maendeleo iweze kutekelezwa.
‘’Mkurugenzi endelea kupambana, tafuta vyanzo vya mapato, tekeleza miradi ukiondoka watakukumbuka, bado tunahitaji vyanzo vipya vya mapato wewe na menejiment endeleni kuumiza akili” alisema byakanwa
Nae mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani amesema kuwa kwa wa fedha wa 2016/2017 Manispaa ilikabidhiwa na kuhojiwa jumla ya 22 na ukijumlisha na hoja za nyuma manispaa ilikuwa na hoja 87 na kati ya hoja hizo 72 zimefungwa na kubakiwa na hoja 15 ambazo zipo kwneye utekelezaji.
Awali akizungumza wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Ibrahim Mdendemi mwakilishi wa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Mtwara alisema kuwa kwa mwaka fedha wa 2016/2017 Manispaa ilipata hati safi (unqualified opinion).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.