Kamati walipotembelea ujenzi wa mfereji wa maji ya mvua kutoka skoya,nabwada hadi mtepwezi wenye urefu wa km 3.4, mradi huu unajengwa na fedha za mkopo kutoka benki ya Dunia ukiwa na lengo la kuondoa adha za mafuriko zinazowapata wananchi wakati wa masika.
Kutokana na utekelezaji nzuri wa miradi ya Maendeleo ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Sekretariet ya CCM Mkoa wa Mtwara iliyoongozwa na Katibu wa CCM Mkoa alhaji Saad Kusilawe imeipongeza Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kutekeleza vizuri ilani ya CCM.
Pongezi hizo zimetolewa leo January 28,2019 katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa ndani ya Manispaa na kuwataka watumishi kuchapa kazi lengo ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanaishi vizuri.
Pamoja na Pongezi hizo Kusilawe amewaomba wananchi kuunga mkono juhudi za serikali kwa kutoa michango yao na kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ili waweze kujipatia maendeleo vizuri.
Amesema kuwa utekelezaji wa ilani ni moja ya nia ya serikali katika kubadilisha Manispaa ya Mtwara ili iweze kuwa jiji hivyo amefurahi kuona ujenzi wa stendi ya mabasi Chipuputa unaenda vizuri na kuwataka wafanyabiashara wanaojenga vibanda vya biashara kujenga kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na mhandisi wa Manispaa.
‘’Nitoe wito kwa wafanyabiashara kujenga kwa maelekezo yaliyotolewa na halmashauri na kwa viwango vilivyotajwa ili tuwe na kituo cha kisasa’’alisema kusilawe
Aidha amewataka wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na stendi kutoa ushirikiano kwa Serikali ili Serikali iweze kufanya kazi yake vizuri.
Kusilawe ametoa rai kwa Mkurugenzi wa Manispaa alipotembelea ujenzi wa soko la kisasa la chuno kutoa nafasi kwa wafanyabiashara wadogo kwa kuwapa sehemu za kufanyia biashara katika soko hilo lengo ni kumkomboa mfanyabiashara mdogo aweze kujikomboa vizuri.
Aidha amesisitiza kutunzwa kwa miundombinu ya soko hilo kwani lengo la CCM ni kuona miradi hiyo inajengwa kwa ufasaha na kwa ukamilifu na kuhakikisha inaisha kwa haraka na katika wakati mwafaka.
Ziara ya ukaguzi wa miradi imehusisha miradi mitatu ikiwemo mradi wa ujenzi wa mfereji mkubwa wa kuondoa maji ya mvua kutoka skoya, Nabwada hadi mtepwezi, ujenzi wa vibanda vya biishara katika stendi ya muda ya mabasi Chipuputa pamoja na ujenzi wa soko la kisasa la Chuno.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.